Get Paid To Promote, Get Paid To Popup, Get Paid Display Banner

M-pesa yazinduliwa Uchumi Supermarket

Posted by dani handrian
Meneja Mkazi wa Uchumi Supermarket Chriss Lenana (kushoto) na Ofisa Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania Hassan Saleh wakikata utepe kuzindua rasmi duka la Vodacom ndani ya Uchumi Supermarket ikiwa ni huduma ya kwanza na ya kipekee nchini. Duka hilo linawawezesha wateja wa Vodacom kupata huduma za kampuni ikiwemo moderm, vocha, usajili wa nambari zao, M-pesa n.k wanapofika kwenye Supermarket hiyo kwa ajili ya kupata kufanya manunuzi ya mahitaji mengine.
Ofisa Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania,Hassan Saleh akiongea na waandishi wa habari mara baada ya uzinduzi wa duka la Vodacom ndani ya Supermarket ya Uchumi. Vodacom imezindua pia huduma za malipo kwa M-pesa kwa wateja wanaofanya manunuzi ndani ya Supermarket hiyo. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim.
Ofisa Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania Hassan Saleh akitumia huduma ya M-pesa kulipia bidhaa alizonunua ndani ya Supermarket ya Uchumi ya jijini Dar es salaam muda mfupi baada ya kuzinduliwa kwa huduma hiyo. Kutoka kushoto ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim, Meneja Mkazi wa Uchumi Supermarket Chriss Linana. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Huduma za Maduka ya Vodacom Upendo Richard.
Ofisa Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania Hassan Saleh akikagua risiti aliyopatiwa baada ya kulipia huduma kwa njia ya M-pesa kwenye Supermarket ya Uchumi ya jijini Dar es salaam muda mfupi baada ya kuzinduliwa kwa huduma hiyo. Kushoto ni Meneja Mkazi wa Uchumi Supermarket Chriss Lenana na Mkuu wa Maduka ya Vodacom Upendo Richard.


Katika muendelezo wa mapinduzi ya kuyaleta maisha kiganjani, sasa wateja wanaofika kupata huduma kwenye SuperMarkert ya Uchumi lililopo katika jengo la Quality Center jijini Dar es salaama wanauwezo wa kulipia huduma zao kwa njia ya M-pesa.

Aidha, Vodacom pia imefungua duka la huduma kwa wateja wake ndani ya Supermarket hiyo ikiwa ni ubunifu wa aina yake hapa nchini na hivyo kuwapa nafasi ya kipekee wateja wa Vodacom kumaliza mahitaji yao yote kwa nwakati mmoja.

“Tunazidi kuongoza katika ubunifu hili ni jambo tunalolipa kipaumbele kw alengo la kuhakikisha tunatoa nafasi kwa wateja wetu kufaidi matumizi ya teknolojia na kubadili maisha yao, hakuna shaka kila tunachokifanya kinawatimiza matarijio yao kwetu.”Alisema Ofisa Mkuu wa Mauzo na Mahusiano wa Vodacom.

Kila mmoja Wakati huu w amsimu wa siku kuu angependa kuona anatumia muda mfupi na kwa urahisi zaidi kupata huduma, hatua moja muhimu ni kuwawezesha kuwa na njia rahisi na nyepesi zaidi ya kukamilisha mahitaji yao na hivyo ndivyo tunavyofanya leo kwa kuwatanagzi wateja wetu kutumia M-pesa wanapofika Uchumi SuperMarket.”Aliongeza

Kwa sasa M-pesa inawaunganisha wateja wetu na biashara zaidi ya 300 katika Nyanja mbalimbali ikiwemo kulipia tiketi za ndege ving’amuzi,LUKU, maji, kutoa na kuweka fedha katika akaunti za benki zaidi ya 20 na hivyo kuongoza soko miongoni mwa huduma za fedha kwa njia ya simu.. Kwa upande wake Meneja Mkazi wa Uchumi Supermarket Tanzania, Chriss Lenana amebainisha kuwa ni jambo la furaha na kujivunia kuzinduliwa kwa ubia huo kati ya kampuni yake na Vodaco na hivyo kuwawezesha wateja wake kutumia simu zao kwa ajili ya malipo ya manunuzi.

“Kufunguliwa kwa duka la Vodacom hapa kwetu kutasaidia sana wateja wetu si tu kuweza kupata huduma za M – PESA bali pia huduma nyingine za kimawasiliano na hatimaye kuepukana na matatizo ya kimawasiliano yanayowakabili. Tunapokea idadi kubwa ya wateja kila kukicha na kwa kufunguliwa kwa duka hili Vodacom wamefanya suala la msingi ambapo awali iliwalazimu wateja kusafiri mpaka makao makuu kufuata huduma hizo kitu ambacho ni usumbufu na kiusalama ni changamoto.” Alisema Lenana.

“Huduma hii ya malipo kwa njia ya M-pesa tutaisamabza kwenye maduka yetu yote ambayoyapo kwenye mipango yetu ya mwaka 2014/2015, ni wazi tumewaptia wateja wetu kitu kizuri na tunawaomba watumie njia hii ya malipo kwa kujiamini kwani mteja hupatiwa pia stakabadhi ya mununizi”Aliongeza.

Duka hilo ni moja kati ya maduka 200 ya Vodacom ambayo yapo mbioni kufunguliwa nchi nzima na pia ni muendelezo wa uboreshwaji wa huduma ya M – PESA na huduma nyinginezo za kampuni hiyo nchi nzima.
 

Copyright © 2009 ikpopped | Design by [blogger merak dua]