Get Paid To Promote, Get Paid To Popup, Get Paid Display Banner

AJAAT YATOA TUZO KWA WANAHABARI

Posted by dani handrian
Mshindi wa Tatu wa Makala za mapambano dhidi ya UKIMWI kwa upande wa magazeti ambaye pia ni Mwandishi wa Gazeti la The Citizen Peter Muthamia(kushoto) akipokea hundi ya shilingi laki tatu (300,000/-) kutoka kwa Mkurugenzi wa Habari na Uraghibishi wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI(TACAIDS) Jumanne Isango(kulia) baada ya kuwa miongoni mwa washindi.
Mshindi wa pili wa Makala za mapambano dhidi ya UKIMWI kwa upande wa magazeti ambaye pia ni Mwandishi wa Gazeti la TanzaniaDaima Hellen Ngoromera (kushoto) akipokea hundi ya shilingi laki tatu na nusu(350,000/-) kutoka kwa Mkurugenzi wa Habari na Uraghibishi wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI(TACAIDS) Jumanne Isango(kulia) baada ya kuwa miongoni mwa washindi.
Mshindi wa nne kwa Makala za mapambano dhidi ya UKIMWI kwa upande wa magazeti ambaye pia ni Mwandishi wa Gazeti la Jamboleo Eben –Ezey Mende(kushoto) akipokea hundi ya shilingi laki mbili na nusu(250,000/-) kutoka kwa Mkurugenzi wa Habari na Uraghibishi wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI(TACAIDS) Jumanne Isango(kulia) baada ya kuwa miongoni mwa washindi.
Mwenyekiti Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari za UKIMWI(AJAAT) Simon Kivamo (katikati) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) jana(leo) jijini Dar es salaam wakati wa kutangaza washindi wa shindano la makala za UKIMWI lilioendeshwa na AJAAT kwa mwaka 2013. Wengine katika picha ni Mkurugenzi wa Habari na Uraghibishi wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI(TACAIDS) Jumanne Isango(kulia) na Meneja Mawasiliano wa AJAAT Perege Gumbo(kushoto).
Mkurugenzi wa Habari na Uraghibishi wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI(TACAIDS) Jumanne Isango(kulia) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) jana(leo) jijini Dar es salaam wakati wa kutangaza washindi wa shindano la makala za UKIMWI lilioendeshwa na Chama cha Waandishi wa Habari za UKIMWI(AJAAT) kwa mwaka 2013. Wengine katika picha ni Mwenyekiti Mtendaji wa AJAAT Simon Kivamo (katikati) na Meneja Mawasiliano wa AJAAT Perege Gumbo(kushoto).Picha na Tiganya Vincent-MAELEZO- Dar es salaam.
 

Copyright © 2009 ikpopped | Design by [blogger merak dua]