Get Paid To Promote, Get Paid To Popup, Get Paid Display Banner

AZAM TV YAANZA RASMI KUTOA HUDUMA ZAKE OFISI KUU JIJINI DAR

Posted by dani handrian
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Azam Media Ltd,Yusuf Bakhresa (kushoto) akikata akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Jengo la Ofisi za huduma kwa wateja za Azam TV, zilizopo kwenye makutano ya barabara ya Nyerere na Mandela, Tazara jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media wa Kampuni ya Azam Media Ltd,Rhys Torrington.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Azam Media Ltd,Yusuf Bakhresa akizungumza na vyombo mbali mbali vya habari vilivyokuwepo kwenye ufunguzi huo wa Jengo la Ofisi za huduma kwa wateja za Azam TV, zilizopo kwenye makutano ya barabara ya Nyerere na Mandela, Tazara jijini Dar es Salaam.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media wa Kampuni ya Azam Media Ltd,Rhys Torrington akisisitiza jambo mbele ya waandishu wa habari (hawapo pichani) juu ya huduma mbali mbali wazitoazo kama Azam TV.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Azam Media Ltd,Yusuf Bakhresa akisalimiana na baadhi ya waigizaji wa Filamu nchini kutoka kundi la (Bongo Movie) waliokuwepo kwenye Ufunguzi huo uliofanyika leo jijini Dar.

 

Copyright © 2009 ikpopped | Design by [blogger merak dua]