Get Paid To Promote, Get Paid To Popup, Get Paid Display Banner

Rais Kikwete afanya uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogovidogo (SIDO)

Posted by dani handrian
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Eng. Omari Jumanne Bakari kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogovidogo (SIDO).

Kulingana na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) Balozi Ombeni Y. Sefue, uteuzi huo umeanza Desemba 04, mwaka huu, 2013.

Eng. Omari Jumanne Bakari ni Mtafiti Mwandamizi katika Tume ya Sayansi na Teknolojia, Dar es Salaam.

Eng. Omari Jumanne Bakari ni Mtanzania mwenye elimu, weledi na uzoefu ambao umemfanya Mheshimiwa Rais aamini kuwa atakapoongoza SIDO, atasaidia kukidhi matarajio ya taifa kwa kueneza ujasiriamali, uwekezaji,uzalishaji na kutoa nafasi za ajira katika ngazi ya viwanda vidogo na vya kati kama msingi imara wa uchumi wa Tanzania, ikiwemo kwa kuingiza sayansi, teknolojia na ubunifu katika viwanda vidogo vidogo.

         “Mwisho”

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
DAR ES SALAAM.
16 Desemba, 2013
 

Copyright © 2009 ikpopped | Design by [blogger merak dua]