Jengo la ofisi, madarasa na library ya Chuo cha Maendeleo ya Utalii Zanzibar liliopo Maruhubi lililofunguliwa na Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe. Seif Sharif Hamad leo Dec 15 2013.
Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe. Seif Sharif Hamad akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Jengo la ofisi, madarasa na library ya Chuo cha Maendeleo ya Utalii Zanzibar ikiwa pia ni miongoni mwa shamrashamra za miaka 50 ya Mapinduzi huko Maruhubi nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Utalii Zanzibar wakimsikiliza Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe. Seif Sharif Hamad (hayupo pichani) katika sherehe za ufunguzi wa Jengo la ofisi, madarasa na library ya Chuo cha Maendeleo ya Utalii Maruhubi nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe. Seif Sharif Hamad akiwahutubia wananchi na wanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Utalii Zanzibar katika sherehe za ufunguzi wa Jengo la ofisi, madarasa na library (kulia) Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk na (kushoto) naibu wake Mhe. Bihindi Hamadi Khamis katika sherehe zilizofanyika Chuoni Maruhubi.
Picha ya pamoja ya Mgeni rasmin Mukamu wa Kwanza wa Rais Mhe. Seif Sharif Hamad Mawaziri mbalimbali na wanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Utalii Zanzibar. (Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).
Na Maryam Fumu Maelezo Zanzibar.
Makamo wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amesema serikali imekuwa na muelekeo mkubwa wa kuimarisha sekta ya Utalii na kuleta mafanikio makubwa yanayoweza kuingiza watalii kutoka nchi mbali mbali duniani.
Alisema Zanzibar inaimarika mwaka hadi mwaka katika sekta hiyo ambapo hivi sasa imekuwa ikichangia wastani wa asilimia 80 ya fedha za kigeni katika kukuza uchumi wa Zanzibar.
Alieleza hayo katika ufunguzi wa jengo la ofisi, Madarasa na Lebrary ya chuo cha maendeleo ya Utalii Maruhubi ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Alisema kuwa serikali ina malengo makubwa ya kuiendeleza sekta hiyo kwa lengo la kuwanufaisha Wazanzibar na kufikia dhana ya utalii kwa wote kupitia katika ngazi zote za wilaya za Unguja na Pemba.
Hata hivyo Maalim Seif amewataka viongozi kufanya juhudi kwa kukiimarisha na kuletea maendeleo Chuo hicho kwa kuweka msimamizi mzuri wa historia ya utamaduni, mila na silka za Wazanzibar ili zienendelee kuchafuliwa.
Pia makamo wa kwanza wa Rais aliahidi kulichukulia hatua barabara liliopo chuoni hapo ili liweze kupatiwa ufumbuzi.
Nae mkurugenzi wa chuo hicho Bi Zuleikha Kombo Khamis amewaomba viongozi kushirikiana na sekta Utalii katika kukijenga chuo hicho katika sehemu ilioharibika ili iweze kuwa na mazingira mazuri.
Aidha Mkurugenzi huyo alisema kuwa changamoto zinazokikabili chuo hicho ikiwemo ukosefu wa barabara pamoja na mmongonyoko wa ardhi sehemu ya nyuma ya chuo hicho linapelekea kuharibu maendeleo ya chuo.
Hata hivyo Bi Zulekha ameshukuru serikali ya awamu ya saba kwa kuwajengea Jengo la Ghorofa mbili jambo ambalo linawapa faraja katika kuleta maendeleo chuoni hapo.